Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Meneja wa sekta ya uchukuzi (NTSA) katika Mkoa wa Nyanza Ezekiel Koech amesema waendeshaji bodaboda katika Kaunti ya Kisii hawazingatii sheria za barabara.

Alisema tabia hiyo huchangia kusababishwa kwa ajali ya kila mara na waendeshaji bodaboda hao.

Hii ni baada ya visa vya ajali kuongezeka katika mji wa Kisii kila wakati na kupelekea abiria wale wanaobebwa kupata majeraha mabaya.

Waendeshaji bodaboda hao kwa sasa wameombwa kuzingatia sheria za barabara ikiwa wanahitaji kuweka maisha ya watu wengine salama, la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza mnamo siku ya Jumatano kwenye hafla ya kuongea na waendeshaji bodaboda hao iliyoandaliwa mjini Kisii, meneja Koech aliwasihi waendeshaji bodaboda kufuata sheria za barabara kila mara na kujali maisha ya wateja wao.

“Naomba kila mwendeshaji bodaboda kuwa na leseni, pikipiki nzuri, helmeti na nguo zito ili kuzuia hewa kali kama njia moja ya kutoweka maisha yako hatarini na kufanya shughuli zenu za uchukuzi kwa njia ya kueleweka,” alisema Koech.

Meneja huyo aliongezea kuwa, ”Ukiwa umevalia nguo isiyo nzito pikipiki ikikuangusha ni wewe utaumia bali siyo pikipiki na tunapowaambia zingatieni sheria za barabara haimanishi tunawasumbua, bali ni maisha yenu tunayaokoa.”

Mtamshi hayo yaliungwa mkono na Kasisi Zachary Bikeri wa Parokea ya Kisii aliyewaomba waendeshaji bodaboda kufuata sheria za barabara. Pia alisema ikiwa idadi ya ajali zitapuguzwa, basi waendeshaji bodaboda sharti wapate mafunzo ya uuendeshaji bodaboda na kuwa na leseni halali.

“Tunahitaji kuwasaidia waendeshaji bodaoda wote ili waendelee kufanya biashara zao bila kusumbuliwa na kufuata sheria za barabara,” alisema Kasisi Bikeri.