Familia moja na mamamboga wameponea kifo baada ya kuhusika katika ajali ya barabara katika barabara kuu ya Kisii-Nyamira siku ya Jumapili jioni.
Ajali hiyo iliyahusisha magari mawili ambayo yalikuwa yakitoka mjini Kisii yakielekea Nyamira, katika eneo la Jogoo Jumapili saa kumi na mbili unusu jioni ambapo gari aina ya Canter la kusafirisha mikate la kampuni ya Sansora lilikuwa likitoka nyuma kwa kasi kasi na katika harakati za kutaka kulipita gari la kibinafsi, likaligonga kwa upande na kusababisha gari hilo ndogo kupotoka barabara na kugonga mama mboga mmoja aliyekuwa akiuza katika kibanda kando ya barabara.
Kwa mujibu wa mama mboga huyo Jane kwamboka, gari la mikate liliiyumba yumba barabarani na kuenda kwa mwendo wa kasi baada ya kugongwa na lori hilo la mikate na kusababisha ajali hiyo ambayo ilimuacha pamoja na mtoto mdogo aliyekuwa karibu na kibanda chake na majeraha makubwa.
Hata hivyo dereva wa gari hilo ndogo ambaye ni mama, alimlaumu dereva wa lori huyo na kusema kuwa alikuwa akiendesha gari kana kuwa alikuwa mlevi.
"Namshukuru Mungu kwa kuniepusha na kifo japokuwa nimepata majeraha madogo," alishukuru dereva huyo.
Mama mboga na mtoto waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya Kisii Level Five kuhudumiwa Maafisa wa Polisi wakiwasili katika eneo la ajali hiyo na kukagua tukio hilo kubaini mwenye makosa. Dereva wa lori alitoroka na bado yupo mafichoni na kuliacha lori hilo kando ya barabara.