Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Utafiti uliyofanywa na Shirika la Kijamii la “National Population Beaural” limebaini kuwa kati ya wanawake wajawazito milioni mbili nchini, asilimia 41 kupata uja uzito bila ya kupanga.

Kulingana na Mshirikishi mkuu wa Shirika hilo eneo la Pwani Margeret Mwaila, hatua hiyo huchangia maafa kwa akina mama wajawazito, na watoto wachanga wanapozaliwa hali ambayo imechangia ongezeko la maafa.

Akizungumza katika kongamano la akina mama la hamasa siku ya Jumatatu eneo la Kisimani mjini Mombasa, Margaret alisema kwamba kati ya watoto laki moja wanaozaliwa kila mwaka hupoteza wazazi wao wakati mama anapojifungua kutokana na ukosefu wa upangaji uzazi.

“Utafiti tulioufanya tumeweza kubaini kwamba asilimia 41 ya wanawake nchini hupata uja uzito bila ya mpangilio, hatua ambayo imechangia wanawake wengi kupoteza maisha yao wakati wakujifungua na hata watoto wao poa hufariki," alisema Mwaila.

Aidha, amewahisi kuzingatia maswala ya upangaji uzaji kwa kuvitembelea vituo vya afya na kupata ushauri nasaha utakaowasadia kumudu ndoa zao na kuwa na familia zenye afya bora.

Kwa upande wake, afisa wa miradi katika Shirika la Afya la DSW George Ouma amewataka wazazi kuvitembelea vituo vya afya ili kupokea ushauri wa upangaji uzazi na kujukumia familia zao vyema ili kufanikisha malezi bora kwa watoto.

“Itakuwa vyema kwa wazazi wote kuvitembelea vituo vya afya kupata ushauri. Sio vyema mzazi wa kiume kumuacha mama aende pekee hospitalini, ni lazima wote wawili muandamane ndio muweze kusaidika kwa pamoja," alisema Ouma.

Viongozi hao wameahidi kuzuru mashinani na kuihamasisha jamii jinsi ya kutambua mbinu mbadala za upangaji uzazi ili kuepukana na maafa wakati wa akina mama wanapojifungua.