Balozi wa Uganda humu nchini Angeline Wapakhabalo ameapa kuimarisha uhusiano mwema kati ya Kenya na nchi yake na koboresha zaidi uwepo wa uhusiano mwema wa kibiashara kati ya nchi za Afrika mashariki.
Balozi huyo amesema kuwa uhusiano wa kibishara ulioko baina ya Kenya na Uganda umeinua uchumi wa nchi yake ambayo utegemea sana bidhaa zake kutoka bandari ya Mombasa, na kusema kuwa nchi ya Uganda inafanya kila inaloweza kupanua nafasi za biashara kati ya serikali hiyo na Kenya.
Akiongea siku ya Jumatano katika hafla ya kuzinduliwa feri mpya huko Likoni, Mombasa, ambayo nchi yake ilinunua kwa kima za zadi milioni mia tatu kutoka kwenye kampuni moja ya humu nchini, Wapakhabalo alishukuru nchi ya Kenya kwa wakati wote kuwa tayari kuifaa nchi yake katika namna zote.
Wapakhabalo alizitaka nchi zote za Afrika mashariki kuonyesha mwelekeo kwa kuja pamoja na kuendeleza uhusiana wa nchi za Kenya, Tanzania, Uganda pamoja na nchi nyingine za maziwa makuu ili kuboresha uhusiano wa kidiplomasia zaidi.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuwa pamoja na kusema umoja na amani unaleta ushirikiano mwema wa kibiashara, na kutoa wito kwa viongozi wa jumuia ya Afrika mashariki kufanya bidii kufanikisha maazimio ya ndoto za wananchi wa nchi zote za Afrika mashariki.