Mwanamume mmoja alifikishwa mbele ya mahakama moja ya Nakuru kwa shtaka la kupatikana na misokoto 30 ya bangi yenye thamani ya Sh600.
Akijitetea mbele ya Hakimu Mkuu, Joel Ng’eno siku ya Jumatano, Peter Kinyongo, alielezea mahakama hiyo kuwa yeye hutumia bangi ili kumchangamsha akiwa kazini.
Mshtakiwa huyo kutoka eneo la makazi ya Bondeni, ambaye ni mpasua mawe katika machimbo ya huko Nakuru, alikiri mashtaka hayo na kuiomba mahakama imsamehe kosa hilo.
Aidha, mshukiwa huyo aliongezea kuwa yeye ndiye anayetegemewa na jamii yake kwa mahitaji ya kimsingi.
Hakimu Ng’eno aliihairisha kesi hiyo na kusema kuwa atatoa uamuzi baadaye.