Familia moja kutoka kijiji cha Nyamokenye eneo wadi ya Kemera kaunti ya Nyamira inaendelea kuhangaika kumfuta msichana wao wa umri wa miaka kumi na sita aliye toweka nyumbani mapema mwezi jana bila kuonekana hadi wa leo. Akizungumza na wanahabari mapema jumapili nje ya boma lake babake mdogo msichana huyo Andrew Makori amesema kwamba msichana huyo alitoka nyumbani mnamo tarehe saba mwezi jana nakuelekea Suneka mahali ambapo alienda kumsalimu shangaziye na kutarajiwa kurejea siku iliyofuatia bila kuonekana. " Sarah alitoka hapa Nyumbani kuelekea kule Suneka kwa minajili yakumtembelea shangaziye na tulitarajia kumuona siku iliyofuatia lakini hakirejea baada yakuaga shangazi na mabinamu zake". Alisema Makori. Makori aliongeza kusema kuwa msichana huyo mwanafunzi wa kidato cha tatu kwenye shule ya Bishop Linus Okoko kule kadongo alikuwa akiongea na watu wasiojulikana kwa njia ya simu usiku huo alipotembelea shangaziye nakuhaidi kuonana nao keshoye lakini shangizi alipomuuliza aliokuwa akizungumza nao msichana huyo alinyamaza. " Shangaziye arituarifu kuwa Sarah alikuwa akiongea na watu kwa njia ya rununu usiku huo alipomtembea na anashuku kuwa huenda msichana huyo alikuwa akiongea na marafiki wake ingawa Sarah alidinda kumwambia ni akina nani alikuwa akizungumza naye". Alisema Makori. Makori sasa anasihii umma ulionaufahamu kuhusu aliko msichana huyo mweupe, mrefu kiasi na mwenye umbo kadri kupiga ripoti kwa kituo chochote cha polisi kilichoko karibu nao ili kwamba waweze wakampata. " Ninasihii umma walio na ufahamu kuhusiana na aliko msichana huyo mweupe na mrefu kiasi na mwenye umbo la kadri kupiga ripoti kwenye kituo chochote cha polisi kilichoko karibu nao ili iwe rahisi kumpa". Alisihii Makori. ....MWISHO....
NYAMIRA
FAMILIA YAHANGAIKA KUMTAFUTA MSICHANA WA KIDATO CHA TATU ALIYE TOWEKA NYUMBANI MWEZI MMOJA ULIOPITA.
ADVERTISEMENT
Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!
Thank you for reading my article! You have contributed to my success as a writer. The articles you choose to read on Hivisasa help shape the content we offer.
-William Maina