Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amewaomba wananchi wa kaunti za Kisii na Nyamira kupea kipau mbele kilimo pamoja na ufugaji ili kuinua uchumi wa kaunti hizo mbili kibiashara.

Gavana huyo alikua akizungumza mnamo siku ya Alhamisi wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kilimo katika uwanja wa michezo wa Gusii.

Aidha, Nyagarama alisema kilimo pamoja na ufugaji vitawezesha kaunti hizo mbili kuinuka zaidi kiuchumi, huku akitoa mfano wa kupanda ndizi ambayo hufanya vyema katika eneo la Kisii pamoja na ufugaji wa ngombe na kusihi watu kukumbatia kilimo zaidi.

“Ikiwa tunahitaji kufikia ruwaza ya mwaka 2030, lazima sisi wakisii tushirikiane pamoja na kufanya kilimo ili ifikapo mwaka huo tupate tayari tumeinuka kiuchumi,” alisema Nyagarama.

Wakati huo huo, gavana huyo aliomba wakaazi wa kaunti hizo mbili kuhudhuria maonyesho hayo ili kujifunza mengi na kutoa mfano wa kufanya kilimo cha kufuga ng’ombe wa maziwa ili kujiendeleza kibiashara na kuinua kilimo katika eneo la Kisii

“Naomba kila mwananchi audhurie maonyesho haya ili kujua yale hajui kuyafanya akiwa nyumbani maana mkaazi akiwa nyumbani hawezi jua jinsi kilimo hufanywa ili kuzaa matunda yaliyo bora,” aliongeza Nyagarama.

Maonyesho hayo yatakamilika siku ya Jumapili tarehe 12 mwezi wa Julai mwaka huu.