Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amesema kuwa wabunge wanaolalamikia uongozi wake ni wale waliomtaka kuwaajiri jamaa zao katika serikali ya kaunti hiyo, jambo ambalo hakulifanya.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika ofisi yake iliyoko mji wa Nyamira, gavana huyo alisema wabunge hao wakiongozwa na seneta wa kaunti hiyo Kennedy Mong’are walimtaka kuwaajiri jamaa zao na akakosa kufanya hivyo.
“Nimekuwa nikiwaita viongonzi hao waje kwa ofisi yangu tuzungumze na waniambie penye nimefanya makosa katika uongonzi wangu lakini hawajawahi fanya hivyo,” alihoji Nyagarama.
“Wiki jana niliwaita na wakokosa kuja hapa Nyamira, kumbe walikuwa na njama ya kuongonza maandamano hii leo, nawakosoa na huo si uongonzi wananchi wa kaunti hii wanatarajia kuwa nayo,” aliongeza Nyagarama.
“Baada ya kukosa kufanya jinsi walivyotaka sasa wanasema niliajiri jamaa zangu pekee na kuacha kuajiri watu wengine,” alidokeza Nyagarama
Viongonzi walioenda hadi ofisi ya gavana kumzungumzia ni miongoni mwao seneta Kennedy Okong’o, mwakilishi wa wanawake Alice Chae, mbunge wa Mugirango maghariibi James Gesami, mbunge wa Mugirango kaskazini Charles Geni, na mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya kumkosa gavana.