Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mhubiri  kutoka kaunti ya Nyamira amewaunga mkono wenzake wanaopinga ndoa za jinsia moja na kuwaomba wakristo wote kutoka kaunti ya Nyamira kuungana pamoja ili kukashifu jambo hilo.

Akiongea Jumanne katika mkutano na wakristo wa kanisa la Matutu PAG lililoko wadi ya Gesima eneo bunge la Kitutu Masaba, Mhuburi Timothy Ogwagwa aliwaomba wakriso wote kuungana pamoja na" kuiombea nchi ya Kenya isije ikakumbwa na masuala ya ushoga ambayo yamekubaliwa katika nchi zingine kama ile ya Amerika."

Alisema kuwa  ushoga kukubaliwa nchini ni kinyume cha Bibilia na tamaduni za Wakenya, alieleza kwamba Mungu aliumba mume na mke ili wawe pamoja.

Ongwaya aliwaomba viongozi wote kutolikubali suala hilo endapo litawasilishwa bungeni huku akimpongeza spika wa bunge la serikali ya kitaifa, Justin Muturi kwa kusema kuwa yeye yupo tayari kutumia wabunge kukataa mambo kama hayo katika nchi ya Kenya .

“Nawaomba viongozi wetu kuyakataa mambo ambayo ni ya aibu katika nchi yetu. Mambo ambayo ni ya kupoteza kizazi kijacho,” alisema.

Kulingana na mhubiri huyo wakristo wako na jukumu kubwa la kuiombea nchi ili isije ikapatwa na majanga kwa sababu ya matendo ya watu.

Waumini waliokuwemo walikubliana na mhubiri wao wakisema kuwa jambo hilo ni la aibu.