Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kamishna wa Kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amekanusha madai ya kusema hajawai shiriki kutatua na kuzuia ujenzi wa kituo cha mafuta kilichoko eneo la Konate, Wadi ya Bonyamatu Kaunti ya Nyamira.

Kituo hicho kimesemekana kilijengwa kwenye chemichemi ya maji ambacho watu hutumia na ni kinyume na sheria.

Hii ni baada ya Wawakilishi wa Bunge la Kaunti ya Nyamira kusema Kamishna huyo hajaonyesha nia yoyote ya kushirikiana na bunge la kaunti hiyo kuzuia ujenzi wa kituo hicho cha mafuta kuendelea katika eneo la Konate tangu ujenzi huo uanze.

Ujenzi wa kituo hicho ulifanyika kinyume na sheria za mazingira nchini huku Wawakilishi wa Bunge la Kaunti ya Nyamira kusema  kamishna huyo alikataa kuamuru maafisa wa polisi kuongoza wakazi wa eneo hilo la Konate kukomesha ujenzi huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari siku ya Ijumaa afisini mwake ilioko mjini Nyamira, kamishna Onunga alikanusha madai hayo na kusema hajawahi pata habari kutoka kwa bunge la kaunti hiyo ya kumwomba kuagiza maafisa wa polisi kuondoa ujenzi huo.

Aidha, kamishna huyo amesema ofisi yake iliomba tume ya mazingira ya NEMA kutatua shida hiyo ya ujenzi wa kituo hicho haraka iwezekanavyo.

Ujenzi wa kituo hicho cha mafuta ulipingwa na Wawakilishi wa bunge la Nyamira waliopitisha mswada wa kuagiza kituo hicho kuondolewa baada ya mswada kufikishwa mbele ya bunge hilo na kiongonzi wa walio wachache katika bunge hilo Jackson Mogusu ambaye alisema maisha ya watu wengi yatakuwa hatarini maana kituo hicho kilikuwa katika chemichei ya maji.

Kamati  iliyokuwa inachunguza ujenzi huo ikiongozwa na mwenyekiti Joseph Magangi ilifikisha ripoti yake kwa bunge hilo siku ya Jumatano na kupendekeza kituo hicho cha mafuta kuondolewa, jambo ambalo Wawakilishi walikubali na kupitisha.