Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Kisii inatarajiwa kuanzisha mradi wa kuweka dawa kwa njia ya kidigitali katika hospitali zote za kaunti hiyo kama njia moja wapo ya kupunguza ukosefu wa dawa hizo katika hospitali.

Akiongea siku ya Alhamisi katika hospitali ya Keumbu wakati wa kuanzisha mradi wa mashine ya upasuaji katika hospitali hiyo, gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae alisema kuwa Serikali ya kaunti ya hiyo imeweka mikakati ya kuanza kuweka dawa kwa njia mwafaka ili wagonjwa wawe wakisaidika wanapohitaji dawa.

"Serikali yangu itaanzisha mradi wa kuweka dawa katika hospitali zote zilizoko katika Kaunti ya Kisii kama njia moja ya kuhakikisha upungufu wa dawa haupo tena,” alihoji Gavana Ongwae.

Gavana huyo alisema kuwa njia hiyo tu ndio itasaidia Serikali ya kaunti ya Kisii kupitia sekta ya afya kujua kama kuna ukosefu wa dawa katika hospitali yoyote ile.

Aidha, Ongwae alisema kuwa wagonjwa wengi ulalamika kuwa kila waendapo katika hospitali hawapati dawa na kuambiwa kununua kwa pesa za kiwango cha juu, lakini sasa njia hiyo itasaidia kubaini kama kuna dawa au la katika hospitali hizo.

Kutokana na madai kutoka kwa wananchi kuwa baadhi ya madaktari huchukua dawa hizo kutoka hospitalini na kuzipeleka kwa duka lao za kibnafsi, Serikali yangu sasa imeamua kuwa njia hii ndio italeta jibu na suluhu kwenye shida hili.