Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi na wanaotumia barabara ya RAM-Prisons mjini Kisii wana sababu ya kutabasamu baada mkurugenzi wa mpangilio wa mji na ardhi Kaunti ya Kisii Moses Onderi kuwahakikishia kuwa tatizo hilo litashughulikiwa hivi karibuni.

Akiongea siku ya Jumatano katika ofisi yake, Onderi alisema kuwa tayari shughuli ya kuchimbua na kutoa vigingi vya miti ambavyo vilikuwa vimefunga mabomba ambazo hupitisha maji chini ya daraja hilo ilishaanzishwa wiki iliyopita na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa daraja hilo limepata suluhu la kudumu.

Pia Onderi aliwataka watumiaji wa barabara hilo kuwa waangalifu wanapowavukisha watu kwenye daraja hilo ambalo limekuwa kero miongoni mwa wakaazi na wanaotumia barabara hilo na kuwasihi wakome kutumia hali hiyo ya kujaa kwa maji kujinufaisha kwa kuwatoza watu pesa nyingi ili kuwavusha kutoka sehemu moja hadi ng’ambo nyingine.

Onderi hatimaye aliwataka wale vijana wanaotumia maji ya mto huo kutotupa uchafu mtoni na taka ambazo zimekuwa zikichangia kuzibika kwa mabomba ambayo yanapitisha maji ya mto huo.

“Tufanye kazi kwa kusaidiana kama jamii na nawaomba wale vijana wanaoyatumia maji yale katika shughuli zao kuacha kutupa takataka majini maanake taka hizo huchangia kufunga mabomba ya maji ya mto huo ambapo husababisha kufurika,” alisema Onderi.