Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Seneta wa kaunti ya Nyamira Kennedy Mong’are Okongo ameomba serikali ya kaunti ya Nyamira kufanya makubaliano na kamati za hospitali zote za kaunti hiyo kabla ya kuanza kufanya ujenzi katika hospitali hizo.

Hii ni baada ya serikali ya kaunti hiyo kuanza ujenzi katika Hospitali ya Manga iliyoko eneo bunge la kitutu Masaba kaunti ya Nyamira kabla ya kufanya mazumgumzo na kamati ya hospitali hiyo.

Akizungumza siku ya Alhamisi katika hospitali hiyo ya Manga seneta huyo alisema ikiwa serikali inataka kufanya ujenzi katika hospitali yoyote ya kaunti, kamati za hospitali sharti zihusishwe ili mambo yatekelezwe kwa njia ya uwazi kukiwa na makubaliano ya pande zote mbili.

“Serikali ya kaunti hii imejaribu lakini mnapofanya ujenzi kwa hospitali, muwe munakaa chini na wanakamati husika ili mkubaliane pamoja,” alisema Okong’o.

Seneta huyo aliweza kutoa usaidizi wa dawa zinazogharimu shillingi millioni moja katika hospitali hiyo.

Wakaazi wa eneo hilo walimshukuru seneta kwa kukumbuka sekta ya afya kwa ununuzi huo wa dawa katika hospitali hiyo huku wakimwomba kuendelea hivyo mpaka watu wa kaunti hiyo kufaidika na huduma za matibabu haswa wanapougua.

“Tunashukuru seneta wetu maana tumekuwa tukisumbuka sana kwa kununua dawa kutoka kwa zahanati lakini sasa seneta wetu ametununulia dawa katika hospitali yetu ya Manga,” alisema Julius Osero, mkaazi.