Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kaunti ya Nyamira na ile ya Bomet imeanzisha mradi wa Sh5m wa kupanua Soko la Chepilat lililoko kwenye mpaka wa kaunti hizo mbili.

Akiongea siku ya Alhamisi wakati wa kupeana mradi huo kwa mwanakandarasi, katibu wa kaunti ya Nyamira Erick Aori alisema kuwa soko hilo la Chepilat litakuwa na manufaa kwa wakazi kutoka sehemu zote za kaunti hizo mbili.

Aori alisema kuwa soko hilo linanuiwa kumalizwa mwezi Machi mwaka ujao na kuwataka wafanyibiashara kuhamia kwingine ili ujenzi uendelezwe bila matatizo yoyote.

“Soko hilo litawafaidi wengi na tayari tumeongea na kaunti ya Bomet jinsi ushuru utakavyokusanywa,” alisema Onchana.

Mwakilishi wa Kaunti ya Bomet Kipkoech Langat alisema kuwa kaunti hiyo itaweka taa za mitaani kwenye soko hilo ili kuhakikisha usalama.

“Baadhi ya sehemu katika soko hilo zilikuwa zimewekwa taa na serikali ya kaunti ya Nyamira na sisi kama kaunti ya Bomet pia tutaweka taa kwa sehemu zilizosalia,” alisema Langat.