Kesi dhidi ya walinzi wawili na jamaa mmoja wanaokabiliwa na shtaka la wizi wa vipuri vya zaidi ya shillingi milioni 1.4 itaendelea mwezi Disemba.
Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkuu wa mahakama ya Nakuru Liz Gicheha baada ya watatu hao kukana shtaka hilo siku ya Jumanne.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa walinzi hao, Michael Nyaika na Leonard Langat, waliokuwa waajiriwa wa Kampuni ya Maize Millers iliyoko Nakuru, kwa ushirikiano na Daniel Kiplangat, waliiba vipuri hivyo vya gari tarehe Oktoba 20,2015.
Watatu hao waliwachiliwa kwa bondi ya Sh500,000 au Sh100,000 pesa taslimu.
kesi hiyo itatajwa tarehe Novemba 12, na kusikizwa tarehe Disemba 3,2015.