Kijana mmoja alifikishwa mbele ya mahakama Nakuru, siku ya Jumanne kwa madai ya kumwiba mbuzi anayedaiwa kuwa mwenye thamani ya Sh12,000 katika eneo la Dundori, Kaunti ya Nakuru.
Dedan Kamau aliyefikishwa mbele ya Hakimu Joel Ng’eno anadaiwa kuiba mbuzi huyo wa John Thuo tarehe Octoba 5.
Mwangi pia anakabiliwa na shtaka la pili la kupatikana na mbuzi huyo wa wizi akijua kuwa alikuwa ameibiwa.
Hata hivyo, Mwangi alikana madai hayo ya wizi na kusema kuwa anasingiziwa.
Licha ya hayo, Hakimu Ng’eno alitilia shaka thamani halisi ya mbuzi huyo huku akiagiza uchunguzi zaidi wa kubaini thamani yake ufanywe ikizingatiwa kuwa bei hiyo iko juu sana.
Mshukiwa aliachiliwa kwa thamana ya Sh12,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa tarehe Octoba 15 na kusikizwa tarehe Novemba 16, 2015.