Kijana wa darasa la chekechea wa umri wa miaka saba aliaga dunia baada ya kugongwa na lori lililokuwa likipeleka kuni kwenye kampuni ya usagaji chai siku ya Jumanne. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na aliyeshuhudia ajali hiyo, dereva wa lori hilo aliliendesha kwa kasi hadi kwenye kituo cha polisi cha Nyamira baada yake kusababisha ajali ili kuepuka ghadhabu za wananchi ambao walitaka kumwangamiza. 

"Baada ya dereva wa lori hilo kugundua kwamba alikuwa amesababisha kifo cha mtoto kwenye ajali aliamua kuliendesha gari hilo kwa kasi hadi kwenye kituo cha polisi cha Nyamira ili kuokoa maisha yake kwa kuwa wananchi wenye hamaki walitaka kumwangamiza," alisema aliyeshuhudia. 

Akithibitisha kifo hicho, afisa mkuu wa polisi kaunti ya Nyamira Ricoh Ngare alisema kwamba polisi walikuwa na wakati mgumu kuondoa mwili huo kutoka eneo la ajali baada ya wananchi wenye hasira kuzua vurugu.

"Polisi walikuwa na wakati mgumu kuondoa mwili huo kutoka sehemu ya ajali kwa kuwa wananchi walizua vurugu, hali iliyosababisha mwili wa marehemu kuondolewa kwenye eneo la ajali baada ya saa tatu, ila kutokana ma ajali hiyo ningependa kuwasihi madereva kuwa waangalifu hata zaidi hasa kwenye msimu huu wa mvua," alisihi Ngare. 

Ngare aliongeza kusema kuwa mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya Nyamira unakosubiri kufanyiwa upasuaji. 

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya ajali nyingine sawia na hiyo kutokea kule Sironga na kusababisha kifo kifo cha mtu mmoja na kuwaacha wengine sita na majeraha makali.