Share news tips with us here at Hivisasa

Kikundi kinachofagia mji wa Kisii kijulikanacho kama 'Minto Youth Group' kimepongeza serikali ya kitaifa kwa huduma ya vijana (NYS), ambao wanaendelea kushirikiana nao kwa kuhakikisha miji yote hapa nchini ni safi.

Wakiongea hii leo, Jumatano katika mtaa wa Jogoo mjini Kisii vijana hao, wakiongozwa na mwenyekiti wa kikundi hicho Kepha Kingo'ina walisema kuwa kikundi hicho kiko tayari kushirikiana na vijana hao wa NYS ili kuhakikisha kuwa mji wa Kisii na viunga vyake ni safi kila wakati

“sisi tuko tayari kushirikiana na vijana hawa ili kuinua viwango vya usafi katika mji wetu kwani ni wajibu wetu kutunza mazingira,” alihoji Kingoina.

Aliongezea kuwa kutokana na kuungana na vijana hao wa hudumu ya NYS kutoka eneo bunge la Kitutu chache Kusini, viwango vya usfi vimeongezeka katika mji wa Kisii, na kusema kuwa wataendelea kushirikiana nao kila wakati.

Kwingineko wameomba wabunge wengine kukubali huduma ya NYS katika maeneo bunge yao ili vijana waweze kupata ajira .

“Tunaomba wabunge wetu kutoka maeneo bunge yote tisa kukubali mradi huu wa huduma ya vijana kwa kuwa utasaidia vijana wengi ambao hawana kazi kupata ajira ili waweze kujiendeleza kimaisha,” aliongeza mkaazi mwingine.