Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kaunti ya Kisii ni mojawapo ya kaunti tano za kwanza kwa maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi humu nchini.

Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa afya katika eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini kaunti ya Kisii Daktari Thomas Oirere.

Akizungumza mnamo siku ya Alhamisi katika eneo la Marani wakati afisa huyo alikuwa anawahimiza wananchi kupimwa ili kujua hali zao za kiafya, Oirere alisema kaunti ya Kisii imekuwa miongoni mwa kaunti ambazo ziko na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa hali ya juu zaidi.

Afisa huyo aliwaomba wale wote tayari wameathiriwa na ugonjwa wa ukimwi kujiandikisha ili kusaidiwa na serikali kwa kukabidhiwa madawa ya kupunguza makali ya virusi hivyo, ili waweze kusukuma maisha wakiwa na ugonjwa huo mwilinini.

Kulingana na afisa huyo, mtu anayefutilia na kuzingatia mashariti yale hupokezwa na madaktari anaweza kuhishi kwa muda mrefu zaidi ikilinganishwa na wale wa kupuuza na kufuata mashariti hayo.

“Uchunguzi ambao umefanywa kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi unaonyesha kuwa kaunti yetu ya Kisii ni mojawapo ya kaunti tano za kwanza kwa kuambukiza virusi hivyo,” alisema Oirere.

“Naomba kila mtu ajue hali yake, na wale ambao wako na virusi natoa wito kuwa waweze kujiandikisha ili kukabidhiwa dawa ambazo zitawawezesha kusukuma maisha mbele,” aliongezea.