Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kituo cha kutetea haki za kibinadamu mjini Eldoret, Centre for Human Rights and Democracy, kimetishia kushtaki kaunti ya Uasin-Gishu kwa madai ya kudhulumu watoto wa kurandaranda almaarufu chokora.

Kituo hicho kilisema haki za watoto wote zapaswa kuheshimiwa kisheria pasipokujali hali ya watoto husika.

Afisa wa utafiti katika kituo hicho Kipkorir Ng’etich alisema kuna ongezeko la dhuluma dhdi ya chokoraa mjini Eldoret.

Akirejelea tukio la hivi maajuzi ambapo baadhi ya watoto hao walidai kusafirishwa kwa lazima hadi nchi jirani na kuachwa huko na maafisa wa usalama wa kaunti

Ng’etich alisema tabia kama hiyo ni unyama wa hali ya juu ambao unapaswa kupingwa. Afisa huyo alisema licha ya watoto hao kuwa chokoraa haimanisha kuwa hawana haki.

“Dhuluma yeyote ile kwa watoto inapaswa kupingwa sheria za watoto hazibagui chokoraa au mtoto mgani, mtoto ni mtoto licha ya hali yake,” alisema Ng’etich.

Kutokana na tukio hilo Ng’etich alitaka utawala wa kaunti hiyo kuomba uma msamaha kwa kudhulumu watoto hao la sivyo shirika lake litachukuklia utawala huo hatua za kisheria.

Kituo hicho kinadai kuwa maafisa wa usalama wa kaunti wamekuwa na mazoea ya kudhulumu chokoraa kwa kuwapiga haswa wakati wanapoendeleza msako dhidi ya chokoraa mjini Eldoret.