Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baada ya serikali ya kitaifa kuamuru shule zote kufungwa kufuatia mgomo wa walimu, mwenyekti wa bodi ya elimu katika kaunti ya Kisii Henry Onderi amesema kufungwa kwa shule kutasababisha baadhi ya wanafunzi kuacha masomo na kuleta hasara katika jamii mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne mjini Kisii, mwenyekiti huyo alikiri kuwa baadhi ya wanafunzi watasahahu masomo na kuacha kuenda shule, na kulaumu serikali kwa kusema kuwa kufungwa kwa shule si suluhisho kwa mgomo.

Wakati huo huo, Onderi alisema serikali inastahili kuheshimu uamuzi wa mahakama na kuwalipa walimu jinsi mahakama hiyo ilivyoamuru.

“Sisi tunashindwa cha kufanya wakati serikali inaendelea kukosea wananchi wa Kenya wakiwemo wazazi, walimu na watoto kwa kufunga shule zote nchini,” alisema Onderi.

“Mara ya kwanza serikali ikaombwa kutuongezea pesa wakakataa, tukaenda kotini tukashinda kesi mahakama ikaamuru walimu wapate nyongeza yao ya mshahara, serikali ikakosa kuheshimu uamuzi wa mahakama kisha baadaye serikali imeona hayo yote imekuwa ikifanya hayatoshi na kuamuru shule kufungwa, kwa nini?" aliuliza Onderi.