Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kikundi cha vijana kutoka eneo bunge la Mogirango Kaskazini wameanza mradi wa kuwahimiza vijana wengine kujiandikisha ili kupata kadi za kupigia kura.

Vijana ambao wanajiita ‘North Mogirango scholars’ wameanzisha shughuli hiyo baada na kugundua kuwa wengi wa wakaazi wa sehemu hiyo hawajui umuhimu wa kupiga kura na wengi wamekuwa hajitokezi kushiriki katika shughuli uchaguzi hasa nyakati za chaguzi kuu.

Akiongea na wanaandishi wa habari siku ya Jumapili katika eneo bunge msemaji wa kikundi hicho Abel Ongeri, aliwataka vijana ktoka sehemu hiyo kujitolea na kuelimisha wenzao umuhimu wa kujiandikisha kupata kadi za kura.

Ongeri alisema kuwa wapo tayari kuwaelimisha wakaazi wote kuendelea hadi mwaka wa 2017 ili kufikia uchaguzi mkuu wawe wafanikisha lengo lao la kuandikisha watu wote ambao wamefikisha umri wa kupiga kura.

"Wakaazi wa eneo hili wakiwa na taarifa na kujua umuhimu wa kujisajili na kupiga kura bila shaka watakuwa na sababu ya kuamka asubuhi na kupigia kura walw viongozi ambao wanafaa," bwana Ongeri alihoji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi hicho Bwana Erick mweresa alielezea matumaini kuhusiana na zoezi hilo akisema kuwa vijana ambao walimaliza kidato cha nne wameonyesha moyo wa kujihusisha na mradi huo.

Alidokeza kuwa hamazisho hilo litawalenga sana kina mama pamoja na vijana ambao wameshika vitambulisho na kuwahimiza wale ambao hawana vitambulisho kuhakikisha kuwa wamejisajili kwa ajili hiyo ili kujiandikisha.