Mwakilishi wa Wadi ya Birongo, kaunti ya Kisii Godfrey Nyamanche amewaomba maafisa wa polisi kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa eneo hilo kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
Hii ni baada ya kubainika kuwa ukosefu wa ushirikiano kati ya maafisa wa polisi na wananchi huchangia utovu wa usalama.
Nyamanche aliema kuwa ushirikiano utazaa matunda ya kuleta usalama na visa vya uhalifu vitapungua kwa asilimia kubwa katika eneo hilo.
Akiongea siku ya Jumapili katika wadi yake wakati mkuu wa polisi wilayani Kisii ya kati Francis Nguri alitembelea wadi hiyo na kutoa gari kwa maafisa wa polisi wa eneo hilo, alisema ni sharti wakazi wajihusishe katika maswala ya usalama.
ambayo itasaidia kuleta usalama pindi wakaazi wanaporipoti kisa chochote cha uhalifu na gari hiyo hutumika kuwapeleka maafisa wa polisi kushuluhisha.
“Naomba maafisa wa polisi muwe mnashirikiana na wakazi wa eneo hili kuleta usalama na mnapopata ripoti yoyote kutoka kwa wakazi, muwe mnakimbia ili kuwaokoa,” alisema Nyamanche.
Aliongeza, “Mara nyingi ugaidi umekuwa ukishuhudiwa katika eneo hili lakini kwa sasa nadhani kila kitu kitakuwa shwari mkishrikiana.”
Mkuu wa polisi wilayani Kisii ya Kati Francis Nguri alisema wale ambao hutekeleza uhalifu siku zao zingali zinahesabiwa.
Aliwaomba wakazi kuasi uovuna kusema kuwa mkono wa serikali ni mrefu na watakabiliwa na sheria na kuchukuliwa hatua kali watakapotiwa mbaroni.
“Mkishuku mtu yeyote kuwa mhalifu naomba mpige ripoti kwa afisi za polisi,” alisema Nguri.