Naibu gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi amewaomba vijana kuchukua vitambulisho kwa wingi katika eneo nzima la Kisii ili kupata fursa ya kutosha ya kuchagua viongonzi wafaao ifikapo mwaka wa 2017.
Akizungumza siku ya Jumatatu katika mji wa Kisii wakati vyama mbalimbali vya vyuo vikuu katika kaunti ya Kisii katika mikakati ya kuanzisha kutembea eneo la Kisii ili kuwahimiza vijana kujiandikisha kuchukua vitambulisho pamoja na kadi za kupiga kura, Maangi alisema ikiwa jamii ya mkisii inahitaji kuchagua viongonzi wazuri sharti wakisii wajiandikishe kwa wingi.
“Jamii ya mkisii ina idadi ya zaidi millioni 2.5 lakini kwa sasa kati ya Kaunti ya Nyamira na Kisii ambazo ziko eneo la Kisii, watu ambao wamejiandikisha ni chini ya watu 800 kumanisha hatuwezi chagua kiongonzi tunayehitaji. Naomba vijana kupata vitambulisho kwa wingi ili tuweze kuwachagua viongonzi tunaohitaji,”alisema Maangi.
Wakati huo huo, Maangi aliomba vijana walio na vitambulisho kuendelea kueneza habari ya umuhimu wa kuchagua viongozi ili wale hawajafanya hivyo wafanye bila taswishi yoyote.
“Jamii ya Meru ina idadi kama ya jamii ya mkisii lakini hao tayari wamejiandikisha watu million 1.4. Kwanini sisi tusijiandikishe kwa wingi? Naomba uandikishaji huo pindi utakapoanza kila mtu ajisajili na wale ambao hawana vitambulisho naomba mujiandikishe kwa wingi,”aliongeza Maangi.