Naibu Gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi ameomba vyombo vya habari kuhakikisha wanatangaza masuala ya kuendeleza serikali za kaunti na wala si mambo ya kuonyesha ulemeveu wa serikali hizo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumanne katika mji wa Kisii, Maangi aliomba vyombo vya habari kutangaza habari za kufahamisha wananchi jinsi maendeleo yamefanywa na serikali za ugatuzi.

“Tunaomba msaada kutoka kwa wananchi wa kushirikiana na viongonzi wa kaunti ili maendeleo yafanyike katika sehemu mbalimbali za mashinani,” alihoji Maangi.

“Serikali za kaunti ni za mhimu sana na zitasaidia wakenya kujiendeleza, naomba ushirikiano wa uwazi ili nchi ya Kenya isonge mbele kimaendeleo,” aliongeza Maangi.

Kwa upande wao, wakaazi walimwomba Maangi kuhakikisha kuwa fedha zinatoka kwa serikali kuu zinatumika vyema.

“Zile pesa tayari ziko kwa hazina ya serikali ya kaunti zifanye maendeleo ili nasi wakenya wa kawaida tunufaike na miradi ya serikali ya ugatuzi,” alisema Joseph Ombiro, mkaazi.

“Pesa zikiongezwa kwa kaunti, miradi mingi itafufuliwa haswa ile imedidimia na itaendelea kutekelezwa katika sehemu zote za nchi ili wananchi wazidi kufurahia matunda ya ugatuzi,” alisistiza Maangi.