Wanafunzi wanaosomea sheria katika Chuo kikuu cha Moi wamepata afueni kwa muda baada ya Mahakama kuu jijini Nairobi kuagiza chuo hicho ifunguliwe hadi pale kesi hiyo itakaposikika.
Katika uamuzi wake aliyotoa Alhamisi wakati wa kusikiza kesi hiyo jaji George Odunga alikaidi uamuzi wa CLE wa kufunga Chuo hicho baada ya kukosa kutimiza kiwango kinachihitajika ya kufunza somo la sheria nchini.
Vingozi wa chuo hicho waliwasilisha kesi hiyo kortini wakitaka isifungwe namna ilivyoagizwa na tume hiyo huku wakiendelea kujadili zaidi.
Kesi hiyo sasa itatajwa tena tarehe 30 mwezi huu huku wanafunzi wakitarajiwa kurejea chuoni humo kusubiri uamuzi utakaotolewa.