Kesi 161 katika mahakama ya Kisii, Kaunti ya Kisii ambazo hazijawahi kukamilika kwa muda mrefu zimetupiliwa mbali ili kupunguza msongamano wa kesi kurundikana katika mahakama hiyo.
Kesi hizo zilitupiliwa mbali siku ya Jumatatu katika mahakama hiyo ilioko mjini Kisii kama njia moja ya kupunguza wingi wa kesi hizo.
Haya yanajiri siku nne tu tangu afisa mkuu katika mahakama ya Kisii Joseph Morema kutangaza kuwa kesi nyingi ambazo ziko katika mahakama ya Kisii ambazo hazijawahi kukamilika zitatupiliwa mbali ili kupunguza msongamano wa kesi katika mahakama hiyo.
Afisa huyo Joseph Morema alitangaza siku ya Alhamisi wiki jana kuwa kesi ambazo zimekaa katika mahakama hiyo bila kukamilika ambazo nyingi zao ni za mwaka wa 2010 kurudi nyuma zingetupiliwa mbali.
Majaji pamoja na mawakili ambao walikuwa na kesi katika mahakama ya Kisii wameombwa kufika katika mahakama hiyo ili kuthibitisha kesi zile zilitupiliwa mbali kama ni kati ya kesi zile wangeshughulikia ili kubaini ukweli.
Ikumbukwe kuwa afisa Morema alisema yeyote aliyekuwa na kesi katika mahakama hiyo ya Kisii afika huko kabla ya kesi hizo kutupiliwa mbali ili kuona ni kati ya kesi zipi hazingeruhusiwa kuendelea.
Aidha, afisa huyo alisema zoezi hilo la kutupilia mbali kesi kutoka kwa mahakama ya humu nchini utafanyika kote nchini.