Mahakama ya Kisii imeongeza mda zaidi kuzuia kituo cha kuuza mafuta kilichoko eneo la Konate kutofanya biashara hadi kesi iliyowasilishwa kortini ikamilike.
Hii ni baada ya kituo hicho cha kuuza mafuta kwa jina Generic Limited kilichoko eneo la Konate, eneo bunge la Mugirango magharibi kujengwa kwenye chemichemi ya maji ambayo watu hutumia, jambo ambalo serikali ya kaunti ya Nyamira na wakazi wa kaunti hiyo walilalamikia na kuwasilisha kesi ili kituo hicho kiondolewe katika eneo hilo.
Mnamo siku ya Jumatatu, wakili steve Mogaka na jaji wa mahakama hiyo John Motingi walikiri kuwa kituo hicho kilijengwa mahala pa chemichemi ya maji, na kutaka mda zaidi ili kukamilsha uchunguzi na kuagiza kituo hicho kutoendelea na biashara ya kuuza mafuta hayo hadi kesi hiyo iliyowasilishwa kortini ikamilike.
Kulingana na Mogaka, maisha ya watu wengi yatakuwa hatarini ikiwa kituo hicho kitaendelea kuuza mafuta, kwani kuna chemichemi ya maji mahala kituo hicho kilijengwa na watu huyatumia
Wakili anayesimamia upande wa mazingira Erastus Getonga alitaka kituo hicho kuzuiliwa kuuza mafuta hayo huku wakiri wa kutetea kituo hicho cha mafuta Bosire Gichana akipewa siku 14 kujibu mashtaka hayo.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 27 mwezi huu. Sasa wakazi wa eneo hilo wanahitaji uwazi uonekane dhidi yao ili kituo hicho cha mafuta kiondolewe katika sehemu hiyo.