Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanaume mwenye umri wa miaka 25 siku ya Ijumaa alifikishwa mbele ya hakimu mtendaji wa Maseno kujibu shtaka ya wizi wa mahindi.

Mathew Muhidi, mkazi wa Maseno alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Philip Oilo kwa kosa analosemekana kutekeleza mnamo Agosti tarehe 1, 2015 mjini Maseno.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, mushukiwa ambaye huuza maji kwa kutumia mkokoteni aliiba mahindi nusu ngunia kutoka kwa kibanda cha mfanyibiashara mmoja mjini humo.

Mahakama ilielezwa kuwa mshukiwa alikua katika pilka pilka za kutembeza maji alipogundua kibanda cha Rosemary Okello hakikuwa na mtu, ilhali bidhaa za kuuza zilikuwa ndani.

Kiongozi wa mashtaka aliongezea kuwa mshukiwa alichukua gunia hilo la mahindi na kuliweka kwenye mkokoteni wake kabla ya kuenda zake.

Korti ilielezwa kuwa Okello aliporejea alikosa gunia ya mahindi yake, kisa ambacho kilimpelekea kuenda kwenye Kituo cha Polisi cha Maseno kuripoti.

Upande wa mashtaka pia ulisema baada ya msako kuanzishwa, askari walifanikiwa kumkamata mshtakiwa akiwa nyumbani mwake akijitayarisha kupeleka mahindi hayo sokoni ili auze.

Mshukiwa aliachiliwa kwa dhamani ya Sh5,000 huku akingojea kusikizwa kwa kesi yake mnamo Septemba tarehe20, 2015.