Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana walioshiriki katika zoezi la kusajiliwa kwa makurutu katika kikosi cha KDF katika eneo la Kisauni kaunti ya Mombasa wamewashtumu wasimamizi hao kwa kuwa na mapendeleo na kukosa kuwa na uwazi katika zoezi hilo lilillofanyika siku ya Ijumaa.

Baadhi ya vijana ambao waliachwa nje kwenye usajili huo walisema kuwa baadhi yao waliweza kusingiziwa kwa vitu ambavyo havikuwa na umuhimu au mojawapo ya vigezo vya kuchukuliwa, na wengine wao kudai kuwa walisingiziwa kuwa hawapo wazima hata kabla ya kuenda kupimwa.

Salma Mwelu, ambaye alikuwa amepita takriban viwango vyote na kubakisha hatua ya mwisho ambayo ni kupimwa kiafya alisema kuwa mmoja wa wasimimazi hao aliweza kumtoa kwa madai kuwa alikuwa anahema sana, na kusema kuwa kuhema kwake kuliashiria kuwa alikuwa na shida ya kifua, kwa hivyo si sawa aende kupoteza muda bure kupimwa na tayari alishajua tatizo lake.

“Mimi waliniweka nje eti nilikuwa napumua sana na kuhema, kwani mtu ukikimbia si unahema, ni tangu lini mafisaa hao wakawa na thibitisho kwa kuangalia mtu na kujua kuwa ana tatizo hata bila kupimwa na wataalam wa afya?” aliuliza kurutu huyo.

Bamison Mwadoe, ambaye pia alikuwa mmoja wa walioachwa, alipendeza kuwa serikali itafute njia mwafaka ambazo vijana watakuwa wanapewa nafasi kwenye jeshi na vikosi vya polisi, na kusema kuwa baadhi ya maafisa waliohusika kuajiri watu walikuwa na jamaa zao ambao walikuwa wamepewa nafasi hata kama walikuja wakiwa wamechelewa.

Ahmed Mwinyi, ambaye amekuwa akishiriki zoezi hilo kwa mara ya tatu sasa, aliwashtumu maafisa hao kwa kumfukuza uwanjani baada ya kuambiwa kuwa hatafaulu kwa sabubu alikuwa anakimbia kwa mwendo wa kinyonga hivyo basi angeweza kupambana na magaidi.

Mmoja wa wale ambao walipenya katika zoezi hilo Josphat Thoya alisema kuwa ijapokuwa kulionekana mapendeleo kwenye zoezi hilo, anashukuru kuwa mwishowe aliweza kupenya.