Mama wajawazito katika kaunti ya Nyamira wamehimizwa kutembelea hospitali za kaunti hiyo kabla ya kujifungua ili wanufaike na huduma kadhaa zilizoko.
Hii ni baada ya uchunguzi kubaini kuwa baadhi ya waja wazito hawatembelei hospitali hadi siku ya kujifungua, na wengine kujifungulia nyumbani.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Alhamisi katika mji wa Nyamira daktari mkuu katika kaunti ya Nyamira Silas Anunga aliwaomba watembelee hospitali ili kuzuia changamoto ambazo huwakumba wakati wa kujifungua kama vile ugonjwa wa Fistula.
“Akina mama wengi hawafiki katika hospitali kujua hali zao na kupewa maelezo jinsi ya kujitunza wakiwa na mimba,” alisema.
Alihusisha visa vya wamama kujifungua kabla yamiezi tisa kukamilika na kutofuatilia kliniki za ujauzito.
alitangaza kwamba wajawazito ambao hawatadudhuria kliniki kama inavyostahili hawatahudumiwa. alisisitiza kuwa vifo vingi vinaweza kuzuiliwa ikiwa watafuata ushauri huo.