Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa ameagiza kuchunguzwa kwa magari matatu madogo yanashukiwa kuuza dawa ya kulevya kwa wanafunzi wa shule katika kaunti hiyo.

Akiongea katika sherehe za kuadhimisha siku ya Mashujaa siku ya Jumanne mjini Mombasa, Marwa alisema kwamba magari hayo yanasafarisha dawa za kulevya katika eneo la Tudor, Majengo na Mji wa Kale.

Kamishna huyo alisema kwamba lazima kwa washukiwa na wamiliki wa magari hayo kutiwa nguvuni na kusitisha kuenea kwa mihadarati katika kaunti hiyo ili kuwanusuru vijana waliyoathirika na mihadarati sambamba na kuzuia kuharibiwa kwa ndoto zao katika siku za usoni.

“Kuna magari hapa Mombasa yanasafirisha madawa ya kulevya na kuwauzia wanafunzi wa shule, hali ambayo inastahili kuchunguzwa na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwani wanaoharibika ni watoto wetu,” alisema Marwa.

Wakati huo huo, waliwashinikiza maafisa wa usalama kuwakabili barabara wale wanaokaidi agizo la maafisa hao la kuwasimamisha magari yao katika vizuizi vya magari ili kuchunguzwa, kwani idadi kubwa ya magari ya kibinfsi husafirisa dawa za kulevya.

Kauli ya Kamishna huyo wa kaunti ya Mombasa imejiri baada ya kampeni ya kukabiliana na ulanguzi na utumizi wa mihadarati kuchacha katika kaunti hiyo ili kuwanusuru vijana walioathirika na janga hilo.