Kesi ya uchochezi inyaomkabili mwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Mishi Mboko ilihairishwa baada ya mashahidi wawili kukosa kuhudhuria kikao cha kesi licha ya wao kufahamishwa mapema kuhudhuria kesi hiyo.
Haya ni kutokana na mwendesha mashtaka Nicolas Kitonga kutoka afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma tawi la Mombasa.
Kitonga aliomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa mwezi mmoja ili apate fursa ya kuongea na mashahidi hao ili kujua chanzo chao cha kukosa kikao cha kesi hiyo.
Wakati huo huo, wakili wa Jerad Magolo aliambia mahakama kuwa wanafanya mazungumzo na afisi ya mwendesha mashtaka pamoja na mashahidi hao kuona iwapo wataendelea na kesi hiyo ama kumuondolea mashtaka mteja wake.
Kulingana na naibu mkurugenzi mkuu wa mashtaka Alexander Muteti, kaunti ya Mombasa Juni mosi mwaka jana katika uwanja wa michezo jijini mombasa mwakilishi huyo alisema maneno haya:
Kwa nukuu “Wakenya wataleta mapinduzi kwa nchi hii, kama ni kutosha imetosha, tumechoka kama Wakenya, mapinduzi yako na watu! Uhuru uko pamoja na watu! Mapinduzi yako pamoja na watu! Nguvu ya watu! Nguvu ya watu! nguvu ya watu”
Kesi hiyo inatarajiwa kusikizwa mwezi ujao.