Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Nyaribari Chache Richard Tong’i amewahakikishia walimu wa shule zote za eneo bunge lake kuwa atafikisha malalamishi yao kwa tume ya mitihani nchini KNEC, kuhusiana na vyeti vya wanafunzi.

Hii ni baada ya walimu kulalamikia tume hiyo kwa kuweka picha za wanafunzi tofauti kwa vyeti vya wanafunzi wengine ambao walifanya mtihani wa kidato cha nne mwaka wa 2013.

Akizungumza mnamo siku ya Alhamisi katika eneo bunge lake wakati alipokuwa na mkutano na walimu wote wa shule za eneo lake, mbunge huyo aliwahakikishia kuwa atafanya awezalo kupata suluhu.

“Nitafikisha malalamishi ya walimu kwa tume ya KNEC ili tume hiyo isije ikarudia kufanya makosa hayo tena,” alihaidi mbunge huyo.

“La kushangaza mno ni wazazi kuombwa shillingi 500 ili vyeti vya wanafunzi wao kuenda kubadilishwa, na hawakufanya makosa hayo, yalifanywa na tume hiyo ya mitihani, hilo nitaenda niulizie,” aliongezea Tong’i.

Aidha, mbunge huyo aliomba walimu kumwandikia majina ya shule zile zilikumbwa na shida hiyo ili awasilishe malalamishi yao.

Naye mwenyekiti wa walimu katika eneo la Kisii ya kati Timothy Atuti alisema kuwa ushirikiano unastahili kuwa wakati bodi za shule zinachaguliwa ili kuchagua watu waliohitimu.