Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Chache Richard Tong’i ameahidi kusaidia shule zote zilizoko eneo bunge lake kifedha ili kuinua viwango vya masomo.

Haya yanajiri baada ya shule nyingi za eneo bunge lake kutuma maombi ya kusaidiwa kifedha ili kubadilisha mijengo ya shule.

Akizungumza siku ya Jumatatu katika eneo bunge lake wakati allikuwa anazikabidhi shule za msingi vitabu, mbunge huyo alisema ikiwa viwango vya masomo vinahitajika kuinuliwa katika kaunti ya Kisii, sharti shule zote zisaidiwe kifedha ili kufanya mabadiliko mbalimbali.

Wakati huo huo, mbunge huyo alisema atajaribu kila awezalo kutafuta wafadhili ambao wataungana naye kushirikiana kusaidia shule hizo.

Tong’i alisema kabla ya kutafuta wafadhili hao, hazina ya ustawi maeneo bunge, CDF, ndio itaendelea kuzisaidia shule hizo kwa ili mijengo ibadilishwe, huku shule nyingi zikiwa na mijengo ya zamani ambayo inastahili kubadilishwa kama njia mojawapo ya kiuinua viwango vya elimu.

“Shule za eneo bunge hili nitajaribu kuzisaidia maana watoto wetu nao wanahitaji mazingira mema ambayo ni ya kuwa kati mijengo mipya, kupata vitabu vya kusoma na mengine mengi. Naomba walimu washirikiane nami ili tuinue viwango vya masomo juu katika shule za eneo bunge langu,” alisema Tong’i.