Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanasiasa kutoka eneo bunge la Nyaribari Chache kaunti ya Kisii Zaheer Jhanda amemkosoa vikali mbunge wa eneo hilo Richard Tong’I, na kumkashfu kwa kutoleta huduma ya vijana almaarufu National Youth Service katika eneo hilo.

Akizungumza siku ya Jumapili katika shule ya msingi ya Ibeno iliyoko eneo bunge la Nyaribari Chache, mwanasiasa huyo alisema Tong’i amefeli kuwajibikia kazi yake vilivyo, na kutaja kuwa bunge hilo liliorodheshwa miongoni mwa maeneo bunge yale hayakufanya maendeleo vizuri.

“Mimi sifurahishwi jinsi uongonzi unavyoendeshwa katika eneo hili, mbona mbunge wetu hakung’ang’ania huduma hiyo ya NYS ili naye apewe fursa hiyo ya kuwaajiri vijana wa eneo hili ?” auliza Jhanda.

Wakati huo huo, mwanasiasa mwingine aliyewania kiti cha ubunge katika eneo hilo Ben Mogaka alitofautiana vikali kuhusu suala hilo, huku akisema huduma hiyo haikuwa inapeanwa kwa kila eneo bunge.

“Maeneo bunge yale yalipatiwa fursa ya kuwaajiri vijana katika huduma ya NYS ni machache, huenda wakati ujao eneo bunge hili letu litapewa fursa hiyo,” alisema Mogaka.

Matamshi hayo hayakumfurahisha Jhanda, huku akishikilia kuwa mbunge wao angefanya Zaidi kuwapa vijana fursa hiyo.