Mhisani mmoja kutoka eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira Robert Osebe amefadhili shule za msingi katika eneo bunge hilo vitabu vya kusoma.
Baadhi ya shule ambazo zilikabidhiwa vitabu hivyo ni shule ya msingi ya Esani, Nyantaro, Nyatieno pamoja na Kebuko, ambazo ziko katika eneo bunge hilo la Kitutu Masaba.
Msaada huu ni baada ya shule hizo kukiri kuwa hazina vitabu vya kutosha, na kuwalazimu kuomba msaada kutoka kwa mhisani yeyoyote, ndiposa Osebe, ambaye ni mwalimu anayestaafu akajitolea kuwasaidia.
Wakati huo huo, Osebe aliwaomba wazazi wote, walimu, wanafunzi na washikadau wengine katika eneo bunge hilo kuungana na kushirikiana pamoja kuhakikisha viwango vya masomo vimeinuka.
“Naomba mwaka ujao nione furaha kwa wanafunzi na kwa wazazi wao wakifurahia matokeo mazuri ya mitihani ili kaunti yetu ya Nyamira iwakilishwe na shule za eneo bunge hili kwa kuifanya vizuri katika mtihani wa kitaifa,” alisema Osebe.
Wazazi wa shule hizo wwalimpongeza Osebe kwa kazi anayoifanya, na kusema kuwa wako tayari kufanya kazi nae ili kuinua viwango vya elimu Zaidi.
“Tunamwomba Osebe aendelee kusaidia shule zetu ili watoto wetu wapate vitabu vya kusoma na wapite katika mitihani,” alisema Beatrice Omariba, mzazi.