Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Kaunti ya Mombasa wanataka kubuniwe mbinu ya kuyaongoza magari katika barabara kuu za mji wa Mombasa ili kupunguza misongamano na kuirahisisha shughuli za uchukuzi na biashara mjini humo.

Wakazi hao, wakiongozwa na Mwanaharakati wa kisiasa na Kiongozi wa Vijana katika eneo la Kisauni Joseph Masai, walisema kwamba kinyume na hapo awali ambapo shughuli za uchukuzi zilikuwa shwari na kuimarika kwa biashara, sasa biashara mjini humu zimeanza kuzoroto.

Akizungumza na mwanahabari huyu mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Masai alisema kwamba misongamano mikubwa ya magari ya umma yanayosubiri kuongozwa na maafisa wa trafiki imetatiza pakubwa shughuli za uchukuzi katika Kaunti hiyo

Aidha, aliwataka maafisa wa trafiki kuibuka na mbinu tofauti ili kuboresha shughuli za uchukuzi katika barabara kuu za mji wa Mombasa pamoja na zile ndogo ili kukuza viwango wa biashara mjini humo.

Masai alidokeza kwamba hali ya usalama katika kaunti ya Mombasa imeimarika na wasafiri hawafai kuhangaishwa na maafisa hao wa trafiki kwani hali hiyo huchangia kushuka kwa uchumi wa kaunti hiyo.

“Maafisa wa trafiki wanafaa kubuni mbinu mbadala za kusitisha misongamno ya magari ya umma katika barabara kuu za Mombasa ili kurahisisha shughuli za uchukuzi na baishara kuimarika baada ya kukumbwa na changamoto za kiusalama,” alisema Masai.