Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Borabu ambao wamekuwa wakihangaishwa na funza hatimaye wamepata sababu yakutabasamu baada ya kampeni inayo ongozwa na mkewe gavana wa Nyamira Bi Naomi Nyagarama kufika katika eneo hilo.

Akiongea katika eneo la Esise kule Borabu siku ya Jumamosi, Bi Nyagarama alisema kuwa kampeni hiyo ina lengo la punguza visa vya wanafunzi kuacha shule kutokana na kuathiriwa na funza.

"Kampeni ambayo tumeianzisha katika eneo hili ina malengo yakupunguza visa vya baadhi ya wanafunzi kuacha shule kutokana na kuathiriwa na funza. Tunataka kuhakikisha kuwa wanafunzi walioacha shule wanapata nafasi yakurejelea masomo yao," alisema Bi Nyagarama.

Bi Nyagarama aidha aliwaomba wahisani kuungana na kampeni hiyo yakuangamiza funza ili kuhakikisha kuwa hali ya watu kuathiriwa na funza imedhibitiwa.

"Ningependa kuwasihi wahisani kuungana nasi kwenye kampeni hii yakutaka kuangamiza funza miongoni mwa watu, kwa kuweka mikakati kabambe yakuhakikisha kuwa hilo linaafikiwa," alisema Bi Nyagarama.

Akizungumzia swala la wanasiasa kuepuka kuzungumzia siasa kila mara kwenye mikutano ya hadhara Bi Nyagarama aliwasihi wanasiasa wenye tabia kama hizo kuungana na viongozi wa kaunti ili kufanya maendeleo kwa minajili ya ustawishaji wa kaunti ya Nyamira.

Wadi ya Nyansiongo na ile ya Esise ni miongoni mwa maeneo yaliyonufaika pakubwa na kampeni hiyo yakuhangamiza funza.