Mkurugezi wa shirika la feri nchini KFS ameahidi kuwa feri mpya ambazo zinaendelea kutengenezwa zitafika mapema mwaka ujao ili kusaidia kuleta nafuu kwenya kivuko cha Likoni.
Musa amesema kuwa bado feri mbili zinaendelea kutengenezwa kwenye nchi moja ya yuropa, na kuna uwezekanao mkubwa kuwa feri hizo zitakuwa zimekamilizwa kuunganishwa kufika mapema mwaka ujao.
Akiwahutubia waandishi wa habari kwenye makao makuu ya shirika hilo huko Likoni baada ya kushuhudiwa patashika ya watu na msongamano mkubwa ambao ulisababisha mkanyagano watu siku ya Jumatatu.
Musa alitoa wito kwa wakazi ambao waliweza kuathiriwa na hali hiyo kuonyesha subira huku mamlaka ya shirika hilo ikifanya juhudi kutatua tatizo hilo ambalo alisema limekwamiza utoaji wa huduma kwa wateja na umma kwenye kivuko hicho cha Likoni.
Alitetea shirika hilo dhidi ya madai kuwa wamezembea akisema kuwa feri zinapokumbwa na matatizo ya ufundi ni jukumu lao kama shirika kuzishughulikia feri ili ziwe katika hali njema ya kutoa huduma bora kwa umma.
Ikumbukwe kuwa zogo hilo lilianza mapema wiki jana siku ya Ijumaa jioni wakati feri mbili ziliharibika na kuwabidi wahudumu kutumia feri moja huku zilizoharibika kufanyiwa ukarabati.
Hata hivyo, maji yalizidi yazidi unga pale ambapo feri mbili zilikumbwa na hitilafu tofauti; moja ikihabika na nyingine kukwama kwenye eneo la maegesho na kusababisha shida hiyo.