Share news tips with us here at Hivisasa

Mahakama ya Kadhi ya Mombasa imemtaka mtalaka wa Mkurugenzi wa bodi ya Nacada tawi la Mombasa Sheikh Juma Ngao kuwasilisha cheti chake cha ndoa ili kesi alioiwasilisha katika mahakama hiyo kuendelea.

Hii ni baada ya mtalaka wake alifika katika mahakama ya Kadhi akitaka kuregeshewa vyeti vyake vya masomo na kitambulisho cha kitaifa anavyodai kuzuiliwa na Ngao.

Santa Rama alisema Juma Ngao amekataa kumrudishia kitambulisho chake cha kitaifa, paspoti pamoja na samani baada ya kutalikiana.

Wakili wa Sheikh Ngao Wallace Cheruiyot alimtaka Santa kuonyesha mahakama cheti cha ndoa ili kuthibitisha kuwa ni mke wake.

Santa alisema kuwa aliolewa na ngao mnamo mwaka 2004 na kumuacha Desemba 2014.

Hata hivyo Kadhi Abdulhalim Hussein alimtaka Santa kuja na cheti cha ndoa pamoja na mashahidi atakaporudi mahakamani.

Kesi itasikilizwa tena Novemba 2 mwaka huu.