Afisa mkuu wa polisi wa Kisii ya kati kaunti ya Kisii Francis Nguri ameapa kuendelea na umwagaji wa pombe haramu katika eneo hilo.
Hii ni baada ya umwagaji wa pombe kuendelea katika sehemu mbalimbali za kaunti ya Kisii kwa siku ya nne mfululizo.
Alikua akizungumza na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumatatu wakati walikuwa wakimwaga pombe katika eneo la Nyamataro lililoko katika eneo bunge la Kitutu Chache Kusini kaunti ya kisii .
Wakati huo huo, afisa huyo aliwashukuru wananchi wa eneo la Kisii kwa ushiriakianao wanaoendelea kuonyesha katika zoezi hilo katika sehemu za kaunti ya Kisii.
“Nawapongeza wananchi wa kaunti ya Kisii kwa uwazi mlio nao kwa kushiriakiana na maafisa wa polisi pamoja na machifu kumwaga pombe ambayo imeonekana kuharibu watu wa kaunti hii na haswa vijana,”alisema Nguri.
Haya yanajiri baada ya Rais Kenyatta kuagiza wakuu wa polisi, machifu na manaibu wao kuhakikisha kuwa ugemaji wa pombe haramu unathibitiwa kote nchini, jambo ambalo limepokelewa kwa njia tofauti.
Kwa upande wa wakaazi hao, uharibifu huo unastahili mno, maana wengi wa vijana na wazee wamepotelea katika maeneo ya pombe.
“Niko katika mstari wa mbele kuunga mkono zoezi la uharibifu wa pombe haramu, maana vijana wetu wangekufa hata kabla ya kuoa, Rais wetu alifanya jambo la maana na tunampongeza sana,” alihoji Gladys Mogonga, mkazi.