Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa afya ya Jamii katika kaunti ya Kisii wameanzisha mradi wa kunyunyuzia dawa za kuwauwa wadudu kama mbu, funza na kunguni kama njia moja ya kutunza mazingira katika shule zote.

Akiongea siku ya Jumatano na Mwadishi huyu katika mji wa Kisii baada ya kuzuru baadhi ya shule na Vyuo haswa zenye bweni,  mhudumu wa afya ya Jamii Kaunti ya Kisii Kepha Kingoina alisema kuwa walianzia shule ya Upili ya wavulana ya Mosocho ili kuhakikisha kuwa wadudu wanaowasumbua wanafunzi hawapo tena katika mabweni.

Aidha, Kingoina amewaomba wasimamizi wa shule zote kuweka ratiba ya kunyunyuzia bweni dawa ili kuangamiza wadudu hao kila wakati.

Kingoina alisema kuwa kutokana na uchafu na kukojoa kwa baadhi ya wanafunzi karibu na bweni ndio huchangia wadudu hao kuingia katika bweni la wanafunzi na kwa sasa amewaomba wasimamizi wote kuwashauri wanafunzi kuzingatia usafi.

“Wadudu kama kunguni huletwa na mazingira machafu na wakati mtu anakojoa karibu na bweni mkojo huchangia wadudu hao kuwa, kwa hiyo nawaomba wanafunzi wote kuzingatia usafi na kukoma kukojoa karibu na bweni lao,” alihoji Kingoina, mhudumu wa afya ya Jamii.

Aidha, alisema kuwa watu wanastaili kufungua milango na madirisha ili hewa safi ipate kufika ndani ya mabweni na vile vile darasani pamoja na kulala ndani ya neti ili kuzuia mbu pia.

Kwingineko Kingoina amewaomba watu wote kushirikiana nao na kuripoti kila wakati wanahitaji usaidii wa kiafya kwani wapo tayari wakati wowote kwa ajili ya kusaidia jamii.