Polisi wa eneo la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu wamemkamata mshukiwa wa uhalifu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mshukiwa huyo alipatikana akiwa katika duka moja katika eneo hilo.

Polisi walisema kwamba mshukiwa huyo anashukiwa kuwa kati ya wale ambao walitekeleza mauaji wa mwanamume mmoja aliyepatikana katika barabara ya Kikuyu-Nairobi akiwa amekatwa katwa na kuuwawa siku ya Jumatano.

Akidhibitisha kisa hiki, siku ya Alhamisi, mkuu wa polisi katika eneo hilo, Mutune Maweu alisema kwamba mshukiwa alishukiwa na afisa wa polisi pale alipoonekana akiwa na wasiwasi baada ya kuwaona maafisa wa usalama.

Alisema kwamba afisa hao walimfuata hadi pale alipoingia katika duka la Wallmart.

Maweu alieleza kwamba polisi walimkagua mshukiwa huyo na kumpata na bunduki bandia aina ya pistol.

“Polisi walimtia mbaroni na yuko katika kituo cha polisi cha Kikuyu huku uchunguzi ukiendelea,” alisema Maweu.