Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume anayekabiliwa na mashtaka ya kulawiti mtoto wa miaka 14 atasalia korokoroni kwa siku tano kusubiri uchunguzi dhidi yake ukamilike.

Hii ni baada ya afisa wa upelelezi Martin Ojwang kuiomba mahamaka siku ya Alhamisi kumpa muda zaidi wakukamilisha uchunguzi wake, kabla ya kumfungulia mashtaka mshukiwa huyo.

Ojwang aleielezea mahakama kuwa mshukiwa, Bonifance Mbuki, anadaiwa kumlawiti kijana huyo tarehe Oktoba 16 katika eneo la Mtongwe huko Likoni na kisha kutoroka.

Mahakama ilielezewa kuwa maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wananchi walifanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa huyo tarehe Oktoba 21, 2015 katika eneo hilo la Mtongwe.

Hakimu Richard Odenyo alikubali ombi la afisa huyo wa upelelezi la kutaka kumzia mshukiwa huyo katika Kituo cha Polisi cha Central mpaka uchunguzi kukamilika.

Kesi hiyo itatajwa tarehe October 26, 2015.