Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Miungano ya kisiasa ya Cord na Jubilee imetakiwa kuacha malumbano ya kisiasa kuhusiana na kesi inayomkabili Naibu wa Rais William Ruto.

Akizungumza katika hafla ya harambee katika kaunti ndogo ya Nyali, kaunti ya Mombasa siku ya Jumapili, aliyekuwa naibu waziri mkuu na aliye kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi alisema cheche za kisiasa zinazoendelea kati ya miungano hiyo miwili inajenga uhasama baina ya wafuasi wao.

Mudavadi aliwataka wanasiasa wa pande zote mbili kuwacha kufanya mzaha na mahakama ya ICC.

Kiongozi huyo pia aliwasuta wale wanaojitokeza sasa kutoa ushahidi wa ni nani aliyepanga njama za kuwafunza na kuwalipa mashahidi wa uongo katika kesi inayomkabili William Ruto.

Mudavadi alisema wale wote wenye ushahidi kuhusiana na kesi hiyo watumie njia za kisheria kuliko maneno ya majukwaani.