Mwakilishi wa Wadi ya Magenche ilioko eneo Bunge la Bomachoge Borabu, Kaunti ya Kisii Timothy Ogugu ameahidi kushirikiana na washikadau wa shule zote zilizoko kwenye wadi yake kuinua viwango vya masomo katika eneo hilo.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika Shule ya Upili ya Magenche katika mkutano wa walimu wakuu wa shule za wadi hiyo ulioandaliwa naye, Ogugu alisema atashirikiana na wasimamizi, washikadau wa shule zote ili kuona viwango vya elimu viimeinuliwa juu zaidi katika wadi yake.
Wakati uo huo, mwakilishi huyo alitumia fursa hiyo kwa kusema atatafuta watu ambao watawasaidia na vitabu vya kusoma ambavyo walimu hao walidai hawana katika shule zao.
Mwakilishi huyo pia aliahidi kuwa atashiriki katika ujenzi wa shule za eneo hilo ili kuona majengo yote mapya yamekamilika ili wanafunzi wapate mahala pa kusomea.
Mwakilishi Ogugu aliwaomba wazazi, walimu, viongionzi na wanafunzi kujiunga pamoja kuona kuwa viwango vya elimu viimeinuliwa zaidi katika eneo hilo.
“Naomba kila upande, iwe niupande wa walimu, wazazi, viongonzi kuja pamoja tushirikiana na wanafunzi ili watueleze ni nini hawana, kile kimekosa katika shule ili tukishughulikie, na hivyo elimu itakuwa ya kufurahisha sana katika wadi yetu,” alidokeza Mwakilishi Ogugu wa Wadi ya Magenche.
Mwakilishi Ogugu aliongeza, “Nitafurahia sana shule za wadi yangu zikipita katika mitihani na ziongoze katika Kaunti nzima ya Kisii, maanake itakuwa shangwe kwangu maana sisi kile tunakihitaji ni elimu kuinuliwa zaidi na kufanya vyema katika eneo hili.”