Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa wadi ya Magenche iliyoko eneo bunge la Bomachoge Borabu, Kaunti ya Kisii Timothy Ogugu amemuomba gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae na naibu wake Joash Maangi kuweka masuala ya kutofautiana kando na kuboresha umoja wa kaunti hiyo.

Hii ni baada ya kudaiwa kuwa viongozi hao wawili wameonekana kutofautiana siku za hivi maajuzi na kuwa hawafanyi kazi pamoja jinsi ilivyokuwa hapo mbeleni.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Kisii siku ya Jumapili, mwakilishi huyo alisema ikiwa viongozi hao wawili hawatafanya kazi pamoja hasa ya maendeleo, basi huenda maendeleo yakarudi nyuma katika Kaunti ya Kisii na wananchi wanaweza kupoteza imani nao.

“Ni vizuri wakati viongozi wako pamoja na kushirikiana kuleta maendeleo dhidi ya wananchi wa kaunti maana viongozi huchaghuliwa kufanya maendeleo kwa wananchi na sio kutofautiana,” alisema Ogugu.

Aliongezea,  “Mimi kama mwakilishi wa wadi katika Kaunti ya Kisii nawomba hao wawili waelewane vizuri na wafanye maendeleo kwa wananchi wa kaunti hii ya Kisii. Sisi hatuhitaji chochote ila maendeleo dhidi ya wananchi.”