Mwakilishi wa wadi ya Gesima Kennedy Nyameino amewaomba wakaazi wa wadi hiyo kushirikiana naye na kuweka siasa kando ili waweze kufanya kazi kwa pamoja na kuinua viwango vya maendeleo,
Akiongea na wakaazi siku ya Jumatano katika eneo la Enchoro, wadi ya Gesima, aliwaomba wakaazi wa wadi hiyo kumuruhusu kuleta maendeleo zaidi kabla ya uchaguzi ujao.
“Nawaomba mshirikiane nami ili niweze kuwa na wakati mwafaka wakuleta maendeleo katika wadi yetu,” alisema Nyameino.
Aidha, alisema kuwa atahakikisha kuwa ametimiza ahadi zote alizotoa wakati wa kutafuta kura kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2017 huku akisema kuwa barabara ya Enchoro-Nyabiosi itakarabatwa hivi karibuni.
“Nimeweka mikakati ya kutosha ya kuhakikisha kuwa barabara hii ya Enchoro-Nyabiosi itakarabatiwa kama njia moja ya kuraihisisha uchukuzi katika eneo hili.
Pia aliwaomba walio na azimio ya kiti cha uwakilishi katika wadi hiyo kutoingiza siasa ya kumuharibia jina kuwa hafanyi maendeleo.
“Mimi kama mwakilishi wenu ambaye ninawawakilisha katika mbuge la Kaunti ya Nyamira ninafanya kila niwezalo ili kuhakikisha kuwa mwanaichi wa kawaida wamefaidika lakini tukiingiza siasa, mambo huaribika na viwango vya maendeleo vitarudi chini,”alisema Nyameino.
Wakaazi waliokuwa katika hafla hiyo walimwomba mwakilishi huyo kutozingatia mambo ya wale wanaotaka kurudisha maendeleo nyuma.
“Wakati mtu amefanya vizuri anastahili kupongezwa na kupewa muda zaidi ili kufanya vyema zaidi,”alisema Lawrence Ochonga, mkaazi.