Kina mama wenye umri wa kadiri wameombwa kujitokeza kwenye afisi za usajili wa watu ili kijisajili kupata vitambulisho vya kitaifa. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea wakati wa kuzinduliwa kwa usajili wa wapiga kura kwenye eneo la uwakilishi wadi lake huko Manga, mwakilishi wa eneo hilo Peter Maroro aliwasihi kina mama na vijana waliomaliza shule kujisajili kupata vitambulisho. 

"Ni jambo la kushangaza kwamba baadhi ya kina mama waliooleka hivi karibuni hawajajisali kupata vitambulisho, ningependa kuwasihi kina mama hao na vijana waliomaliza shule kujitokeza kujisajili kupata vitambulisho vya kitaifa," alisihi Maroro. 

Mwakilishi huyo aliongeza kwa kusema kuw tayari bunge la kaunti ya Nyamira lilikuwa limeiomba afisi ya usajili wa watu kufanya usajili kwenye vituo tamba ili kuhakikisha kwamba idadi kubwa ya watu wamejitokeza kujisajili kupokea stakabadhi hizo mhimu.

"Sisi kama bunge tayari tumeiomba afisi ya usajili wa watu nyamira kufanya usajili wa watu kwenye maeneo tamba ili kuhakikisha idadi kubwa ya watu," alisema Maroro. 

Kulingana na Maroro, usajili wa vitambulisho ni mhimu kwa kuwa huwasaidia watu kupata huduma mhimu za kiserikali, huku akiongezea kusema kuwa itawawia vigumu watu kupokea huduma za serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali bila ya vitambulisho. 

"Usajili wa vitambulisho ni kitu mhimu sana kwa kuwa bila ya kuwa na kitambulisho, mtu hawezi pata huduma mhimu za serikali na hata pia mashirika yasiyokuwa yakiserikali," alisema Maroro.

Mradi huo wa usajili unatarajiwa kuendeshwa kwenye wadi zote 20 za kaunti ya Nyamira.